Daniel 9:20-23

20 aBasi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Bwana Mwenyezi Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu, 21 bwakati nilipokuwa bado katika maombi, Jibraili, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibu wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. 22 cAkanielimisha na kuniambia, “Danieli, sasa nimekuja kukupa akili na ufahamu. 23 dMara ulipoanza kuomba, jibu lilitolewa, ambalo nimekuja kukupasha habari, kwa maana wewe unapendwa sana. Kwa hiyo, tafakari ujumbe huu na uelewe maono haya:

Copyright information for SwhKC